FAIDA YA NDIZI MBIVU KIAFYA
Ndizi ni miongoni mwamatunda yenye ladha nzuri Ndizi hupendwa na watu wengi duniani kote, Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama "SUNCROSE" ,"FRUCROSE" na "GLUCOSE" na kiasi kingi cha nyuzinyuzi yani "FIBER" ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni. Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wakuongeza na kuimarisha Nishati ya mwili,ambapo ulapo tunda hili unaweza pata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakula walau ndizi mbili tu na kwakua na sifa hiyo tuanaweza sema Ndizi ni tunda muhimu sana kwa wana michezo.- Nishati siyo faida pekee utakayo hipata kwa kutumia Ndizi kwakua ni tunda lenye uwezo wa kuponya na kuzuia mfadhaiko wa Akili (depression) kwakua Ndizi ina kirutubisho kinacho julikana kama (Tryptophan) ambayo nia aina ya protini inayotumika kuhufanya mwili kuwa na utulivu
- Ndizi pia huwasaidia wanawake wanaopata matatizo wakati wa hedhi,hivyo wanashauriwa endapo wanasumbuliwa na tatizo hilo kutumia Ndizi wakati wa hedhi kula Ndizi mbivu inaweza kuponya.
- Ndizi husaidia kupambana na Anemia, kwakua Ndizi ina madini ya chuma "IRON" ambayo ni mazuri katika mwili na inaweza kusaidia watu wenye tatizo la Anemia,Anemia niungonjwa unao sababisha upungufu wa chembechembe za damu,hivyo kwakua madini hayo ya chuma yanaongeza uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini (RED BLOOD CELLS)
- Ndizi husaidia kukabiliana na tatizo la shinikizo la damu kwakua Ndizi ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium na ndio chanzo kikuu pia cha potassium na wakati huo huo pia Ndizi hina kiasi kidogo cha chumvi "SODIUM" yani Ndizi ni SOLUBLE na INSOLUBLE, hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (STROKE) kwa binadamu.
- Ndizi husaidia Afya ya ubongo hii ni kwa sababu utafiti unaonyesha kuwa potassium inayo patikana kwa wingi husaidia kuimarisha uwezo wa kufikiri kwa kuwa misuli ya kichwa kufanya kazi vizuri
- Ndizi ni moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unao tokana na ulevi wa jana (HANGOVER) hivyo unaweza kunywa"Milk Shake" iliyo tengenezwa na Ndizi na kutiwa Asali, Ndizi hutuliza tumbo ikisaidiwa na Asali,inayorejesha kiwango cha sukari kilicho pungua kwenye damu.
- Pamoja na hayo ndizi pia husaidia katika kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kuongeza Nguvu za kiume na nguvu ya mwili kiujumla,na kutuliza vidonda vya tumbo,kushusha joto mwilini na kurekebisha mapigo ya moyo
ZINGATIO;usitumie ndizi kama umegundulika na ugonjwa wa figo kwakua Ndizi mbivu uzalisha kiwango kikubwa cha potassium/ hosha ndizi kabla ya kula unaweza kula mda wowote kabla ya chakula na baada ya chakula
USISAHAU KUFATILIA KURASA ZETU
INSTAGRAM @AFYA_NA_MATUNDA_
FACEBOOK @ HABARINAAFYA
EMAIL info.afyanamatunda@gmail.com
contacts +255684559098. / +255764500827
* you're health is my priority*
No comments:
Post a Comment