Friday, March 13, 2020


                   FAIDA YA NDIZI MBIVU KIAFYA
  • Ndizi ni miongoni mwamatunda yenye ladha nzuri Ndizi hupendwa na watu wengi duniani kote, Ndizi ina aina tatu za kipekee za sukari zinazojulikana kitaalamu kama "SUNCROSE"  ,"FRUCROSE" na "GLUCOSE" na kiasi kingi cha nyuzinyuzi yani "FIBER" ambazo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni. Pia tunda hili linaelezwa kuwa na uwezo mkubwa wakuongeza na kuimarisha Nishati ya mwili,ambapo ulapo tunda hili unaweza pata nishati ya kufanya kazi ya muda wa dakika 90 endapo utakula walau ndizi mbili tu na kwakua na sifa hiyo tuanaweza sema Ndizi ni tunda muhimu sana kwa wana michezo.
  • Nishati siyo faida pekee utakayo hipata kwa kutumia Ndizi kwakua ni tunda lenye uwezo wa kuponya na kuzuia mfadhaiko wa Akili (depression) kwakua Ndizi ina kirutubisho kinacho julikana kama (Tryptophan) ambayo nia aina ya protini inayotumika kuhufanya mwili kuwa na utulivu
  • Ndizi pia huwasaidia wanawake wanaopata matatizo wakati wa hedhi,hivyo wanashauriwa endapo wanasumbuliwa na tatizo hilo kutumia Ndizi wakati wa hedhi kula Ndizi mbivu inaweza kuponya.
  • Ndizi husaidia kupambana na Anemia, kwakua Ndizi ina madini ya chuma "IRON" ambayo ni mazuri katika mwili na inaweza kusaidia watu wenye tatizo la Anemia,Anemia niungonjwa unao sababisha upungufu wa chembechembe za damu,hivyo kwakua madini hayo ya chuma  yanaongeza uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini (RED BLOOD CELLS)
  • Ndizi husaidia kukabiliana na tatizo la shinikizo la damu kwakua Ndizi ina kiwango kikubwa cha madini ya potassium na ndio chanzo kikuu pia cha potassium  na wakati huo huo pia Ndizi hina kiasi kidogo cha chumvi "SODIUM" yani Ndizi ni SOLUBLE na INSOLUBLE, hivyo kulifanya kuwa tunda bora katika kupambana na tatizo la kupanda na kushuka kwa shinikizo la damu na kupatwa na kiharusi (STROKE) kwa binadamu.
  • Ndizi husaidia Afya ya ubongo hii ni kwa sababu utafiti unaonyesha kuwa potassium inayo patikana kwa wingi husaidia kuimarisha uwezo wa kufikiri kwa kuwa misuli ya kichwa kufanya kazi vizuri
  • Ndizi ni moja ya dawa ya haraka ya kuondoa uchovu unao tokana na ulevi wa jana (HANGOVER) hivyo unaweza kunywa"Milk Shake" iliyo tengenezwa na Ndizi na kutiwa Asali, Ndizi hutuliza tumbo ikisaidiwa na Asali,inayorejesha kiwango cha sukari kilicho pungua kwenye damu.
  • Pamoja na hayo ndizi pia husaidia katika kutuliza mishipa ya fahamu, kuondoa wasiwasi, kuongeza Nguvu za kiume na nguvu ya mwili kiujumla,na kutuliza vidonda vya tumbo,kushusha joto mwilini na kurekebisha mapigo ya moyo
ZINGATIO;usitumie ndizi kama umegundulika na ugonjwa wa figo kwakua Ndizi mbivu uzalisha kiwango kikubwa cha potassium/ hosha ndizi kabla ya kula unaweza kula mda wowote kabla ya chakula na baada ya chakula

USISAHAU KUFATILIA KURASA ZETU
INSTAGRAM @AFYA_NA_MATUNDA_
FACEBOOK  @ HABARINAAFYA

EMAIL info.afyanamatunda@gmail.com

contacts +255684559098. / +255764500827

                * you're health is my priority*


Thursday, March 12, 2020


FAIDA YA TIKITIMAJI KIAFYA




Tikitimaji ni tunda linalo pendwa,Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa nichanzo kikuu cha protein,fat, carbohydrates, nyuzinyuzi, calcium, phosphorus,iron, potassium, magnesium,carotene na vitamin C A B6 na virutubisho vingine vingi

Virutubisho na Madini hayo yote ni muhimu katika afya ya mwili
Tikitimaji linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wakuimalisha misuli ya mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu
Tikitimaji huboresha Afya ya macho kwakua tunda hili lina potassium na vitamin A ambayo husaidia misuli ya macho hivyo ufanya kusaidia kuwa na uwezo wakuona
Tikitimaji Huimarisha Kinga ya miwili kwa vile hili zaidi ya Asilimia 12 ya vitamin C na moja ya sifa ya vitamin C kujenga na kukinga mwili hivyo Tikitimaji kusaidia kuimarisha kinga ya mwili
Tikitimaji husaidia afya ya ubongo madini ya kopa yanayo patikana kwenye tunda hili kwaiyo ina nafasi kubwa kusaidia ubongo kufanya kazi vyema
Tikitimaji ni chanzo cha madini ya potassium. Tikitimaji husaidia kuondoa sumu mwilini kwakua tikitimaji ina tunda lenye vitamin C na kwakua ina acid ascorbic ambayo ufanya kazi kama kiosha sumu mwilini
Tikitimaji husaidia mtiririko wa damu kwakua tikitimaji ni chanzo cha madini ya potassium ambayo kazi yake ni kusaidia misuli kuwa imara upelekea damu kutiririka vizuri
Pia Tikitimaji hubadilisha protein kuwa Nishati
vilevile Tikitimaji huponyesha majeraha na kukinga uharibifu wa seli vitamin C nichanzo kikuu cha ulinzi na kikanga hivyo upelekea mwili kuwa nakinga
Tikitimaji husaidia mmeng'enyo wa chakula  vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa ajili ya kufanya mmeng'enyo wa chakula uende vizuri,na kwakua nyuzinyuzi pia upatikani kwa wingi kwenye Tikitimaji
Tikitimaji maji hulinda afya ya moyo kwakua tikitimaji maji ni chanzo cha potassium na madini ya potassium yanayo patikana kwenye Tikitimaji ni muhimu sana katika utendaji kazi wa misuli ya moyo
Tikitimaji husaidia afya ya meno na fizi kuwa imara na madini ya calcium, Folate yanayo patikana ni muhimu kwa kusidia mifupa kuwa imara hivyo kutumia Tikitimaji
Tikitimaji husaidia kuongeza maji mwilini kwakua asilimia 92 ya tunda hili ni maji
Tikitimaji ni muhimu kwa wajawazito kwakuwepo kiasi kikubwa cha potassium na vitamin C na B6 ambazo ni muhimu kwa afya ya ukuaji wa mtoto, hivyo mama mjamzito anashauriwa kutumia tunda hili.

ZINGATIO; unashauriwa kula na mbegu zake zingatia mazingira ya kulitumia jitahi kuliosha kbla ya kula

KWA USHAURI PIGA +255684559098 +255764500827

USISAHAU KU LIKE NA KU FOLLOW KURASA ZETU
INSTAGRAM @ AFYA_NA_MATUNDA_

https://www.facebook.com/pg/habarinaafya/reviews/

written by HAMIS BASHIR Instagram @iamkimtu

          * you're health is my priority*


FAIDA ZA ZABIBU KATIKA AFYA
zabibu ni matunda yenye faida nyingi kiafya na kwa mwili pia zabibu ina virutubisho vingi

NISHATI
WANGA
KAMBA KAMBA
MAFUTA
PROTEIN
VITAMIN B1,B2,B3,B5,B6,B9,C,E,K
CALCIUM
IRON
MAGINIZIAMU
MANGANIZI
SODIAMU
POTASSIUM
FOSFORASI

Hivi vyote ni madini na virutubisho muhimu katika mwili wa binadamu

FAIDA ZABIBU KIAFYA

KUTIBU PUMU
zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu

HUIMARISHA MIFUPA
Madini ya shaba ,chuma,manganizi, hupatikana kwa wingi kwenye zabibu,na madini haya husaidia kujenga mifupa imara

Huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda pia husaidia mafuta kuto kulundikana kwenye mishipa ya damu
zabibu ina kampaundi za flavonoids aina za resverotory ambayo husaidia kutoa sumu mwili
hivyo hayo yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na shinikizo damu

zabibu zina viondoa sumu yani (antioxidant) ambayo husaidia kuondoa sumu yani free radicals kutoka kwenye figo.pia hupunguza tindikali ya uric acid kwa kuongeza kiasi cha mkojo unao tengenezwa na figo
zabibu ina uwezo wa kupunguza lehemu mbaya (cholesterol) kwenye damu zabibu zina kampaundi kama pterosostilbini ambazo hupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu,pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza lehemu kutoka kwenye utumbo

zabibu hupunguza hatari ya kupata kansa
kampaundi za resverotory huondoa sumu zinazo weza leta saratani pia baadhi ya kampaundi nyingine huzui seli za saratani kukua na kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili

HUSAIDIA AFYA YA MOYO
HUBORESHA MMENG'ENYO WA CHAKULA
HUONGEZA NGUVU ZA MWILI
MUHIMU KWA WAJAWAZITO

MUHIMU:-WAKATI WAKUTUMIA HIKIKISHA UNAOSHA KWA MAJI YA UVUGU VUGU VIZURI KUTUMIA WAKATI WOTE KUTUMIA KAMA JUISI AU KULA KAMA KAWAIDA

USIKOSE KUTUFATILIA KWENYE PAGES ZETU MBALI MBALI:- INSTAGRAM@AFYA_NA_MATUNDA_

FACEBOOK PAGE @AFYA NA MATUNDA
/HABARINAAFYAhttps://m.facebook.com/story.php?story_fbid=113360723613504&id=111997310416512

EMAIL:- Info.afyanamatunda@gmail.com

CONTACTS US:- ±255684559098
                              +255764500827

PERSONAL PAGE INSTAGRAM @Iamkimtu

          you're healthy is my priority